
Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi…………………
SEHEMU A (Alama 15)
UFAHAMU
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Jambo moja kubwa katika mambo ya huzuni kwa watu wote sasa lilitokea. Mke wangu mpenzi
alishikwa na maradhi, na baada ya muda kidogo wa udhaifu na maumivu akafariki dunia.
Utengano huu kati yetu ulitokea baada ya miaka kumi ya kuishi pamoja kwa mapenzi, amani,
raha na baraka. Tukio hili lilikuwa pigo kubwa sana kwangu na msiba mkubwa katika nyumba
nzima. Marehemu huyu alikuwa tunu ya maisha yangu, tegemeo na mshauri mwema.
Alinisaidia katika mambo mengi wakati wa maisha yetu pamoja ambayo yangalinishinda
kuyatenda mimi peke yangu.
Sura yake ilikuwa jamali kwa kimo cha kadiri, uso ulikuwa mviringo wa yai, nywele nyeusi za
kushuka, paji pana, nyusi za upindi, macho mazuri yalikuwa na tazamo juu ya kila kitu kope za
kutana, masikio ya kingo yasiyopitwa na sauti ndogo, meno ya mwanya yaliyojipanga vizuri
mithili ya lulu katika chaza, ulimi wa fasaha na maneno ya kiada yaliyotawaliwa, midomo imara
isiyokwisha tabasamu. Sauti pole na tamu kama wimbo, kiedevu cha mfuto katikati yake
palikuwa na kidimbwi kidogo. Shingo kama mnara ambayo juu yake paliota kichwa cha mawazo
mengi, chini ya shingo mabega yalikuwa kama matawi ya maua, kifua cha madaha, mikono ya
mbinu, tumbo jembamba na miguu ya mvungu. Uzuri wake ulikuwa kamili. Kwa tabia alikuwa
mwaminifu na mfano wa kuiga katika nyumba.
Wanawake ni wengi kama walivyo wanaume lakini wenye sura kama iliyoelezwa ni adimu sana
kukutana nao duniani. Kabla ya kuoa nililitafuta umbo namna yake muda wa miaka kumi. Kitu
nilichokuwa nikitafuta kwa muda wote mwisho nilikipata, lakini baada ya miaka kumi mingine
kilikwenda safari ya watu wasikorudi na wito usiofika. Mauti yake ya mapema yalikuwa ni
msiba na hasara kubwa sana kwangu. Nilishindwa kujizuia kama nilivyotaka, machozi yalinitoka
mengi sana na yalikuwa hayazuiliki sababu ya pigo zito lililonijia.
Maswali
(a) Andika kichwa cha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi matano.
……………………………………………………………………………………………....
……………………………………………………………………………………………....
……………………………………………………………………………………………....
……………………………………………………………………………………………....
(b) (i) Ni jambo gani kubwa liletalo huzuni kwa watu wote lililomtokea mwandishi wa
habari hii?
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
(ii) Ni muda gani mwandishi wa habari hii aliishi na mkewe baada ya harusi yao?
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………