
Namba ya Mtahiniwa …………………
SEHEMU A (Alama 25)
UFAHAMU
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Katika miji mikubwa nchini Tanzania wimbi la ongezeko la watu bado ni kubwa. Ongezeko hilo
la watu limesababisha kuzuka kwa matatizo makubwa maeneo ya mijini ikiwemo msongamano
mkubwa wa magari na watu. Hali hii imesababisha wafanyakazi kuchelewa kazini, wanafunzi
kuchelewa shuleni na hata wagonjwa kuchelewa kufikishwa katika vituo vya kutolea huduma za
matibabu.
Hebu tujiulize, kwa nini watu wengi wanaondoka vijijini na kukimbilia mijini? Majibu yanaweza
kuwa mengi, lakini miongoni mwa majibu hayo inaweza ikawa huduma zisizokidhi mahitaji ya
kijamii. Jamii inatarajia kupata huduma bora za maji, umeme, barabara, matibabu, ajira na
mawasiliano. Jamii inaposhindwa kupata huduma hizo katika maskani yao, lazima itafute
huduma hizo nje. Na njia pekee ni kukimbilia mijini ambako huduma hizo zinapatikana.
Anasa pia ni sababu mojawapo. Ikumbukwe kuwa kundi kubwa la watu wanaokimbilia mijini na
vijana. Kundi hili ni la watu wanaopenda starehe, hawataki kujituma na kujikwamua kimaisha,
wanapenda kupata mafanikio ya haraka. Vijana wengi wanakimbilia mijini jambo ambalo
linaleta wasiwasi wa hali ya maisha katika maeneo hayo ikilinganishwa na rasilimali zilizopo.
Wengi wao hujiingiza katika vitendo vya uhalifu kama wizi na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Ongezeko la watu mijini husababisha makaszi duni, uchafuzi wa mazingira na uhalifu wa kila
aina. Ongezeko la watu katika maeneo ya miji linakwenda sambamba na ongezeko la magari
hivyo tatizo la miundombinu isiyokidhi pia hujitokeza. Hali hii ikiachwa iendelee uharibifu wa
mazingira utaongezeka kwa kiasi kikubwa kwa sababu watu watatafuta njia mbadala ili kuzitatua
changamoto zinazowakabili.
Maswali
(a) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu hiki cha habari.
(i) Msongamano ………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
(ii) Maskani ……………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
(iii) Miundombinu ………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………