Namba ya mtahiniwa …………………………... JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA PILI 021 KISWAHILI Muda: Saa 2:30 Jumatatu, 16 Novemba 2015 asubuhi Maelekezo 1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E. 2. Jibu maswali yote. 3. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa. 4. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi. 5. Vifaa vyote vya mawasiliano haviruhusiwi katika chumba cha mtihani. 6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia. KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU NAMBA YA SWALI ALAMA SAINI YA MTAHINI 1 2 3 4 5 JUMLA
Namba ya mtahiniwa …………………………... SEHEMU A (Alama 15) UFAHAMU 1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata: Wakati wa ukoloni mabepari wa Kijerumani walianzisha kilimo cha pamba huko Kusini mwa Tanzania. Waliwalazimisha Wamatumbi kufanya kazi katika mashamba yao. Pamba iliyopatikana ilipelekwa Ujerumani. Kama anavyosema kibarua mmoja aliyeteswa na mabepari hao, " Wakati wa kilimo kulikuwa na dhiki sana. Sisi vibarua tuliokamatwa tulikaa mstari wa mbele, tukilima. Nyuma yetu kulikuwa na mnyapara, kazi yake kutupiga kwa mijeledi. Nyuma ya mnyapara alikuwepo jumbe, na kila jumbe alisimama nyuma ya watu hamsini. Na nyuma ya majumbe alisimama Bwana Kinoo mwenyewe. Lo! Hapo shuhudia kifo." Mjerumani alipofika nchini akaamrisha Wamatumbi kulipa kodi. Watu walimjibu, "Hudai kitu. Hatuna deni kwako. Ikiwa wewe mgeni unataka kukaa nchi hii basi ni lazima wewe utuombe sisi. Na sisi tutakuambia utoe sadaka kwa Miungu wetu. Wewe utatoa chochote na sisi tutaifanyia karamu Miungu kwa niaba yako; tutakupa ardhi na wewe utakuwa na mahali pa kukaa. Lakini siyo sisi wenyeji tukupe wewe sadaka. Hilo haliwezekani hata kidogo." Juu ya dhiki zote walizopata yaani dhiki ya njaa, dhiki ya maonevu, dhiki ya kulimishwa na kupigwa, watu walistahimili wakavumilia kwa sababu hawakuweza kupigana, kwani hawakuwa na umoja. Vilevile walijua kuwa nguvu ya Mjerumani ilikuwa kubwa. Wakangoja. Katika mwaka wa 1904 akaja mtume, jina lake Kinjeketile. Karibu na kwao Ngarambe kulikuwa na bwawa la maji kaitika kijito cha Mto Rufiji. Kinjeketile alipandwa na pepo aitwaye Hongo, aliyekuwa akikaa katika bwawa hilo. Kinjeketile aliwafundisha Waafirka maana ya umoja, akawapa moyo kwa nguvu ya maji. Waafrika wakawa na umoja na nguvu. Watu wengi waliosikia jina lake walikuja kumuunga mkono. Maswali (a) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano. (b) Eleza wazo kuu linalojitokeza katika habari uliyoisoma. (c) Ni mambo gani yanayothibitisha kwamba ni kweli Wamatumbi waliteswa? Taja mambo matatu. (i) (ii) (iii)
Namba ya mtahiniwa …………………………... (d) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari ulichosoma. (i) Mnyapara (ii) Mijeledi (iii) Walistahimili (iv) Sadaka (v) Mtume (e) Ni mambo gani mawili unayojifunza kutokana na habari hii? (i) (ii) (f) Fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu kwa maneno yasiyozidi 40. SEHEMU B (Alama 15) UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI 2. (a) Kwa kauli zifuatazo andika KWELI kwa kauli iliyo sahihi au SIO KWELI kwa kauli isiyo sahihi. (i) Kazi ya fasihi ni moja tu na ni ile ya kuelimisha jamii. (ii) Kiunganishi ni neno ambalo huunganisha dhana mbili tu. (iii) Elekeza, shikilia, shikamana, maelekezo, mshikamano, tolewa, nitakutolea, ondokeni ni maneno yaliyoundwa kutokana na mnyumbuliko (iv) Methali ni usemi wenye pande mbili (v) Kitendawili ni aina ya fumbo lisilotumia lugha ya picha lakini hudai jibu (b) Andika tungo zifuatazo kwa usahihi: (i) Mwalimu mkuu amewakilisha mada katika mkutano. (ii) Nilikwenda mjini nikamkutana Maria. (iii) Habarini zenu mabibi na mabwana. (iv) Kila siku nafanyaga kazi.
Namba ya mtahiniwa …………………………... (v) Kwa kuwa sina gari nitakwenda na miguu. (c) Andika mifano ya kauli zinazoonesha muktadha wa rejesta zifuatazo; (i) Hotelini (ii) Mahakamani (iii) Dukani (iv) Darasani (v) Hospitalini SEHEMU C (Alama 15) SARUFI 3. (a) Nyumbua maneno yafuatayo na kuunda maneno manne kwa kila neno. (i) Angalia (ii) Chukua (iii) Oga (iv) Kata (v) Omba (b) Tumia maneno yafuatayo kama nomino na utunge sentensi moja kwa kila neno: (i) Starehe (ii) Ukweli (iii) Utaalamu (iv) Umoja (v) Uzembe (vi) Ukarimu (vii) Ushujaa (viii) Upweke (ix) Upendo (x) Furaha
Namba ya mtahiniwa …………………………... (c) Kitenzi kikuu huweza kutumika sambamba na kitenzi kingine kukamilisha sentensi. Katika sentensi zifuatazo bainisha vitenzi vilivyotumika. Sentensi ya kwanza ni mfano: (i) Aliyekuja atasafiri kesho. TS T (ii) Mgeni wangu amekwisha kuwasili. (iii) Amina hakuataka kumuudhi. (iv) Mafundi wangali wanashona viatu. (v) Wataendelea kumsubiri hadi kesho. (vi) Gari lilikuwa limeharibikia mlimani Kitonga. SEHEMU D (Alama 40) FASIHI SIMULIZI 4. (a) Eleza kwa kifupi maana ya dhana zifuatazo: (i) Shairi (ii) Vichekesho (iii) Ngonjera (iv) Visasili (v) Mapingiti (b) Jaza nafasi iliyoachwa wazi kukamilisha methali zifuatazo: (i) Samaki mkunje (ii) njaa mwana malegeza. (iii) hutanda na kuyeyuka. (iv) Ajidhaniaye kasimama (v) usiilalie mlango wazi.
Namba ya mtahiniwa …………………………... (c) Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata: Mwanafunzi ikibali, mbele ya wako mwalimu. Katika siku si mbali, utakuwa aalimu. Kijitia baradhuli, baadaye ulaumu, Mbele ya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali. Usijifanye kiburi, kujifanya chakaramu. Hiyo wanaita shari, ndani yake ina sumu, Hivi hauna habari, heshima kitu adimu, Mbele ya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali. Katika hii sayari, namba moja ni elimu, Usiipate sufuri, kisha hapo ulaumu, Maisha haya safari, mwana ujenge timamu, Mbele ya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali. Katika hii sayari, namba moja ni elimu, Usiipate sufuri, kisha hapo ulamu, Maisha haya safari, mwana ujenge timamu, Mbele ya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali. Ni walezi mashuhuri, hivyo wana umuhimu, Wameishika nambari kutokana na kalamu, Usimwendeshe chuchuri, uidumishe nidhamu, Mbele ya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali. Mwalimu baba na mama, hilo wazi ufahamu Hivyo tazama ndarama, zisisababishe ghamu, Neno hili la zama, shika nakupa jukumu, Mbele ya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali. Sitapenda kukuchosha, kwa mengi kukushutumu, Nakutakia maisha, ya hsule yenye utamu, Ili upate bashasha, na mema kutakadamu, Mbele ya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali. (i) Mtunzi wa shairi hili anatoa ujumbe gani?
Namba ya mtahiniwa …………………………... (ii) Ni mambo gani matatu ambayo mwanafunzi unatakiwa kuyaepuka kama yalivyoelezwa katika shairi ulilosoma? (iii) Bainisha kituo bahari katika shairi ulilosoma. (iv) Bainisha vina vya kati na vya mwisho vya shairi ulilosoma. (v) Mshairi ana maana gani anaposema, “Neno hili ni la zama, shika nakupa jukumu.” (vi) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi ulilosoma; Ikibali Baradhuli Kutakadamu Chuchuri Bashasha 5. Unatarajia kwenda kumtembelea shangazi yako aitwaye Nakijwa aishiye Ikwiriri Rufiji. Andika barua kwa shangazi kumjulisha makusudio yako. Jina lako liwe Jaja Okwi, Shule ya Sekondari Ndorwe, S.L.P 1534, Kilomeni, Mwanga.
Namba ya mtahiniwa …………………………...