
SEHEMU A (Alama 15)
1. Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika kilili chetu, umechaguliwa kusoma risala kwa
Mgeni Rasmi. Soma risala hiyo kisha jibu maswali yanayofuata.
Ndugu Mgeni Rasmi,
Mustakabali wa taifa letu na raia wake upo katika hati hat] iwapo half iliyopo sasa miongoni mwa
viongozi wetu tuliowapa dhamana kubwa ya kuliongoza taifa hill haitadhibitiwa. Ubinafsi uliokithiri,
rushwa, ufisadi ubadhirifu wa mall ya umma, uhujumu uchumi, jambazi, dhuluma, utapeli, mauaji ya
imani za kishirikina na uovu wa kila aina umekuwa ndio sera yao. Dhamira njema ya ukombozi wa
wananchi kufikia maisha bora kwa kila Mtanzania itakuwa ndoto za alinacha tu kama hautakuwepo utashi
wa dhati wa kisiasa wa kupambana na hall hiyo.
Ndugu Mgeni Rasmi,
Jambo la kuSikitisha ni kuendelea kukua kwa kasi pengo lililipo baina ya wenye nacho na wasionacho;
yaani matajiri na maskini katika jamii inayoamini katika misingi ya usawa wa binadamu. Katika jamii hii
ya tabaka la wakulima na wafanyakazi; wapo watu wenye fedha nyingi wanaishi maisha ya kifahari sana
na kuwaacha wengine wengi ambao hata kupata mlo kamili wa siku ni shida. Wengi hawana ajira za
kuaminika wala mitaji au elimu ya ujasiriamali, wakijaribu kukopa mikopo midogo midogo wafanye
biashara ill kujikwamua kiuchumi, Lakin' wapi! Wametumbukia katika la umaskini uliokithiri. Maisha
yamekuwa ya samaki baharini. Samaki mkubwa kumla mdogo!
Ndugu Mgeni Rasmi,
Vita juu maadui wakubwa wa jamii yetu, ujinga, umaskini na maradhi imekuwa ni nadharia tu. Vifo vya
wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano vimeongezeka. Kipato cha Mtanzania kinazidi
kushuka na thamani ya fedha yetu halikadhalika. Utandawazi ulikusudiwa kutupatia wajomba kwa jina
maarufu "wawekezaji" iii waje kutukwamua kiuchumi. Wote tuliweka matumaini ya kukua kwa uchumi
na kuongezeka kwa nafasi za ajira katika viwanda, migodi, mashamba, mabenki, mashirika na
makampuni katika sekta binafsi. Hata hivyo hall si ya kuridhisha; wajomba wengi "wanatula visogo",
Wanakula vyetu huku wanatung'ong'a. Wanawasainisha waheshimiwa wetu ya ulaghai, na wanatumia
udhaifu uliomo ndani ya mikataba hiyo kuhamisha utajiri wetu kwenda kwao. Madini, mbao hata
wanyama! Maskini, wajinga ndio waliwao. Usimwamshe aliyelala usije ukalala wewe.
Ndugu Mgcni Rasmi,
Leo hii kumeanza kuzuka migogoro ya kugombea ardhi; baina ya wakulima na wafugaji, wawekezaji na
wanavipp na viongozi na raia. Mahali pengine kama vile kule Kilosa damu ilimwagika. Hii si dalili nzuri
kwa mustakabali wa taifa letu, amani yetu tuliyojivunia kwa kitambo sasa Ltilaiwvka rehani. Ukiona
vyaelea vimeundwal.
Ndugu Mgeni Rasmi,
Hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha. Dalili ya mvua ni mawingu. Dalili za kuzinduka kutoka katika
usingizini mzito zinaanza kuonekana. Tumeanza kufuta matongotongo. Hoja za kuhoji na hatimaye
kukubali kuirejea baadhi ya mikataba tuliyoingia kichwa kichwa inayoonesha kila dalili za kiwingu cha
rushwa ni hatua ya kujivunia. Mapambano dhidi ya ufisadi na uimarishaji wa demokrasia na miundo
mbinu ya nchi ni hatua ya mafanikio. Wabunge bila shaka mtaendelea kuisaidia serikali na sekta binafsi