
8.
Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Mchezo wa jana wa mpira wa miguu ulikuwa patashika nguo kuchanika. Katika
kutupia macho wachezaji wa Tunisia, ni dhahiri kuwa mtazamaji yeyote angeweza
kutabiri kuwa wachezaji gani wangejipatia ushindi. Wachezaji wa Tunisia walionekana
kuwa majitu ya miraba minne na hivyo kutabiriwa kuwa washindi wa mchezo huo.
Kwa siku za nyuma, wachezaji wa timu ya Tanzania waliweza kwenda sare na timu ya
Tunisia kwa kipindi chote cha mchezo na pengine havwakuweza kupata ushindi kabisa.
Kutokana na hilo, hofu kubwa ilitanda miongoni mwa Watanzania kwani siku hiyo
huenda historia ikajirudia ya kufungwa au kutoka sare. Kipenga kilipolia wachezaji wa
pande zote mbili walijitupa uwanjani wakionesha utanashati na manjonjo mengi huku
wakipiga mazoezi ya hapa na pale. Watu walipowashangilia kwa hoi hoi na vitijo
waliongeza madaha yao. Haukupita muda mrefu walitengana na kila mmoja alikwenda
katika sehemu yake na mara kipenga cha kuashiria mpira kuanza kikapigwa. Naam,
ilianza vuta nikuvute, kila mmoja akiwania kuanza kuufumania mlango wa mpinzan1
wake. Kukuru kakara hiyo iliendelea hadi mwisho wa kipindi cha kwanza ambapo
hakuna aliyefanikiwa kugusa nyavu za mwenzie. Kwa kipindi hiki chote timu ya
Tanzania ilionekana kupiga moyo konde na kuwania ushindi. Wachezaji wa Tunisia
nao waliapa kutoshindwa kuwatoa Watanzania kama walivyotazamia.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila mehezaji kujihami dhidi ya adui yake ili mradi kila
mmoja apate nafasi ya kuutundika mpira wavuni. Hata hivyo wachezaji wengi wa
pande zote walionekana kulowa kwa kutoelewa nini kitatokea mbele yao baada ya
dakika arobaini na tano zilizofuatia.
Muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza, timu ya Tunisia iliona lango la timu ya
Tanzania na kujiandikia bao la kwanza. Uwanja mzima ulipooza kwa upande wa
Watanzania lakini Watunisia walionekana kufunguka nyuso zao kwa bashasha.
Waswahili wanasema, "Mungu si Athumani." Hivyo, ilipotimia dakika ya themanini
va mchezo, Mohamedi Kajole alipata nafasi nzuri, akautoma mkwaju mkali kinywani
mwa lango la
Tunisia na
kuiandikia timu ya
Tanzania goli la
kusawazisha. Nderemo.
shangwe, vifijo na
vigelegele vilitawala uwanjani kwa kuwa Kajole aliwatoa
Watanzania aibu katika kiwanja cha nyumbani.
Mchezo
ulikuwa kama
umepata mvuto na ari
mpya kwa
wachezaji wa
Tanzanja ambao
walionekana kuwa na
kasi
kubwa
katika
kupasiana mpira.
Wachezaji wa
Tunisia
walianza
kuhangaika
uwanjani
wakijua
kuwa
ushindi
karibu
utatoweka
mikononi san
Mashabiki
wa
Tanzania nao
walishika kasi
katika
kushangilia timu
yao.
Harakati hizo
zilizaa
matunda
katika
dakika ya
themanini na
tisa
pale
Kassim
Kanombe
alipoipatia timu
yake ya
Tanzania goli la
ushindi.
Vifijo. hoi
hoi na
shangwe
zilitawala
uwanjani kwa
upande wa
Watanzania. Lakini
mambo
havakuwa
mazuri kwa
upande wa
timu ya
Tunisia
kwani
walichokitegemea
hawakukipata.
Hadi
mwisho wa
Ukurasa wa 5
kati ya 7
csee2023