Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE 021 KISWAHILI (Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni) Muda: Saa 3 Mwaka: 2020 Maelekezo 1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12). 2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, maswali matatu (3)kutoka sehemu C. 3. Sehemu A in alama kumi na tano (15),sehemu B alama arobaini (40)na sehemu C ina alama arobaini na tano (45). 4. Zingatia maelekezo ya kila sehemuna ya kila swali. 5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwikatika chumba cha mtihani. 6. Andika Namba yako ya Mtihanikatika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia. Ukurasa wa 1 kati ya 5
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org SEHEMU A (Alama 15) Jibu maswali yotekatika sehemu hii. 1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia. (i) Ni neno lipi linalotoa taarifa kuhusu nomino? A Kitenzi C Kivumishi B Kielezi D Kiwakilishi E Kiunganishi (ii) Katika lugha ya Kiswahili kuna aina ngapi za vitenzi? A mbili B C sita D tano tatu E nne (iii) Maneno yepi kati ya yafuatayo yametokana na lugha za Kibantu? A Kitindamimba na bendera B Hela na mtutu C Kitivo na ngeli D Godoro na sharubati E Bunge na shule (iv) Ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kuteua maneno na miundo ya tungo wakati wa mazungumzo? A Mada, muktadha na mazungumzo ya ana kwa ana. B Mada, mazungumzo na uhusiano wa wazungumzaji. C Mada, muzungumzaji na muktadha wa mazungumzo. D Mada, mzungumzaji na uhusiano wa wazungumzaji. E Mada, muktadha na uhusiano wa wazungumzaji. (v) Bainisha kauli inayoonesha dhima muhimu za vitendawili katika jamii: A Kuhimiza umoja na ushirikiano. B Kupanga watu katika marika yao. C Kuchochea udadisi wa mambo. D Kuchochea uwongo wa mambo. E Kukosoa wadadisi wa mambo. (vi) Njia mojawapo ya kuzuia utata katika lugha ya mazungumzo ni ipi kati ya zifuatazo? A Kuepuka makosa ya kisarufi na kimantiki. B Kutumia neno lenye maana zaidi ya moja. C Kutumia kiwakilishi kiambata katika neno. D Kuweka msisitizo au ufafanuzi zaidi. E Kutumia mofimu sahihi za wakati. Ukurasa wa 2 kati ya 5
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org (vii) “Waandishi wa fasihi huzungumzia watu wenye mienendo isiyokubalika katika jamii ili kukemea mienendo hiyo.” Katika tamthiliya ulizosoma, ni wahusika wepi kati ya wafuatao wana mienendo isiyokubalika? A Joti, Ngoswe na Mama Furaha. B Padri James, Ngoswe na Baba Anna. C Mazoea, Mama Furaha na Joti. D Ngoswe, Baba Anna na Suzi. E Ngoswe, Joti na Padri James. (viii)Kati ya sababu zifuatazo ni ipi si sahihikuhusu matumizi ya kamusi? A Kujifunza lugha ya kigeni. B Kusanifisha maneno mapya. C Kubaini kategoria ya neno. D Kujua maana za maneno. E Kujua tahajia za maneno. (ix) Ni methali ipi inayokinzanana methali “Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu?” A Manahodha wengi, chombo huenda mrama. B Palipo na wengi, hapaharibiki neno. C Haba na haba, ujaza kibaba. D Kidole kimoja, hakivunji chawa. E Fimbo ya mnyonge, ni umoja. (x) Bainisha sentensi ambatano yenye muundo wa sentensi changamano mbili kati ya sentensi zifuatazo: A Gari lililomteka tumeliona na dereva aliyetekwa ameonekana. B Mtoto aliyeumia jana amelazwa na mtoto mwingine hajitambui. C Mpe haki yake yote ili nae akupe haki yako yote. D Uchunguzi uliofanyika juzi umezaa matunda. E Baba anataka kujenga nyumba lakini mama hataki kabisa. 2. Oanisha maana za vipera vya Fasihi Simulizi katika Safu Ana dhana za Fasihi Simulizi zilizo katika Safu B,kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia. Safu A Safu B (i) Sherehe au shughuli zinazofanywa na jamii katika kipindi A Utani maalumu cha mwaka. B Matambiko (ii) Masimulizi ya mambo ya kishujaa ambayo mtu amewahi C Miviga kuyafanya maishani mwake. D Harusi (iii) Maigizo mafupi yaliyojaa ucheshi na mzaha. E Ngoma (iv) Sadaka itolewayo kwa miungu au mahoka. F Majigambo (v) Masihara wanayofanyiana wanajamii wakati wa shida na raha. G Vichekesho Ukurasa wa 3 kati ya 5
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org SEHEMU B (Alama 40) Jibu maswali yotekatika sehemu hii. Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org 3. Ainisha maneno yaliyokolezwa wino katika tungo zifuatazo: (i) Wangapiwaliondoka mapema leo? (ii) Wachezaji wangapiwatashiriki kwenye mechi ya kwanza? (iii) Wanangu wapendwa niwaeleze mara ngapimpate kunielewa? (iv) Wawakilishi wote waliungamkono hoja ya mbunge wa Kusini Unguja. 4. Eleza kwa ufupi mazingira manne ambayo kielezi huweza kujipambanua, kisha tunga sentensi moja kwa kila aina ya mazingira. 5. Eleza maana mbili kwa kila tungo zifuatazo: (a) Mama anaota. (b) Tafadhali nipe sahani ya kulia. (c) Vijakazi wanalima barabara. (d) Amekanyaga mtoto. 6. Kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Takadiniliyoandikwa na Ben J. Hanson (MBS), eleza kwa kifupi madhara manne yanayoweza kutokea katika jamii iwapo itaendekeza mila potofu ya kuwabagua walemavu wa ngozi. 7. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata katika kijitabu cha kujibia. Chawa huyo ni kinyozi, mtia wembe kichwani, Ndiye huharibu ngozi, anapokata fashini, Chawa ni huyo mkazi, uliyenaye jirani, Usimdhanie mbuzi, huyo yuko majanini, Wala usidhani funzi, umuonaye shambani, Hawa hawana ujuzi, wa kukunyoa mtani, Panapouma ufizi, sumu hutoka kinywani, Wapi hutokea nzi, kama si pako chooni, Chawa aliye kichwani, ni huyo kinyozi wako. Chawa unapomuona, upesi muweke dole, Usimwache kunona, mpaka azue kelele, Jitahidi kumbana, akatokomee mbele, Ukimwacha kutuna, atakutia upele, Usije kula dona, na katafuta mchele, Chawa usimpe jina, abaki akutawale, Ukianza kujikuna, mtafute kwenye nywele, Na nguoni hujibana, mkame kama nyenyele, Chawa aliye kichwani, ni huyo kinyozi wako. Maswali (a) Kwa kutumia mfano, fafanua mtindo uliotumika katika shairi hili kwa kutoa hoja mbili. Ukurasa wa 4 kati ya 5
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org (b) Mwandishi anamaanisha nini anaposema, “Chawa unapomuona, upesi muweke dole?” (c) Eleza kwa ufupi kuhusu mtazamo wa mtunzi wa shairi hili. (d) (i) Andika methali moja inayosadifu shairi hili. (ii) Kwa kutumia maneno yako eleza jinsi shairi hili linavyoendana na maisha halisi ya jamii zetu. 8. (a) Eleza kwa kifupi tofauti ya msingi kati ya barua ya mwaliko na tangazo. (b) Andika tangazo la kumtafuta ndugu yako wa kiume anayeitwa Masana Madale ambaye amepotea. SEHEMU C (Alama 45) Jibuma maswali matatu (3)kutoka katika sehemu hii. 9. Kwa kutumia aina nne za vyombo vya habari vilivyopo nchini hivi sasa, onesha mchango wa kila kimoja katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. ORODHA YA VITABU USHAIRI Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP) Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP) Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD) RIWAYA Takadini - Ben J. Hanson (MBS) Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P) Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P) TAMTHILIYA Orodha - Steve Reynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC) Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH) 10. Kauli za washairi ni nyenzo muhimu katika ujenzi wa jamii bora. Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika diwani mbili ulizozisoma. 11. “Jamii ya kitanzania inakabiliwa na matatizo mbalimbali ya kijamii yanayokwamisha maendeleo. Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma. 12. “Waandishi wa kazi ya fasihi hulenga kuleta mabadiliko katika yale wanayoyaandika.” Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma, tetea kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila kitabu. Ukurasa wa 5 kati ya 5