Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE 021 KISWAHILI (Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni) Muda: Saa 3 Alhamisi, 07 Novemba 2019 mchana Maelekezo 1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12). 2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, maswali matatu (3)kutoka sehemu C. 3. Zingatia maagizo ya kila sehemuna ya kila swali. 4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwikatika chumba cha mtihani. 5. Andika Namba yako ya Mtihanikatika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia. Ukurasa wa 1 kati ya 6
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org SEHEMU A (Alama 15) Jibu maswali yotekatika sehemu hii. 1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia. (i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa? A Kiunganishi B Kivumishi C Kihisishi D Kiwakilishi E Kielezi (ii) Ni sentensi ipi hainakitenzi kisaidizi? A Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa mtiifu. B Watoto wanatakiwa kulala mapema ili wawahi shuleni. C Paka alikuwa anataka kula chakula cha mbwa. D Juma alikuwa anasoma kitabu cha hadithi za mapenzi. E Robert Kelly anataka kuja kutumbuiza mwezi Desemba. (iii) Ni seti ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi? A Vitu, mahali, wanyama, binadamu, fanani na maleba. B Hadhira, wanyama, maleba, binadamu na fanani. C Hadhira, binadamu, wanyama, vitu, mahali na fanani. D Fanani, vitu, mahali, binadamu, maleba na wanyama. E Wanyama, manju, binadamu, vitu, mahali na maleba. (iv) Bainisha seti ya maneno inayofaa kuingizwa kwenye kamusi kwa kuzingatia mpangilio wa alfabeti. A Jabali, jadhibika, jabiri, jadi, jalada B Jabali, jabiri, jadhibika, jadi, jalada C Jabali, jadi, jadhibika, jalada, jabiri D Jabiri, jabali, jalada, jadi, jadhibika E Jabali, jalada, jabiri, jadhibika, jadi (v) Ni sifa ipi haitofautishi fasihi simulizi na fasihi andishi? A Ukubwa B Uhifadhi C Uwasilishaji D Ukuaji E Ueneaji (vi) Jozi ipi ina vipengele sahihi vinavyounda umbo la ndani la kazi ya fasihi simulizi? A Falsafa, muundo, ujumbe, wahusika B Mandhari, msimamo, ujumbe, dhamira C Ujumbe, mtazamo, migogoro, dhamira D Ujumbe, msimamo, dhamira, wahusika E Lugha, mgogoro, falsafa, mtindo Ukurasa wa 2 kati ya 6
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org (vii) “Ng’ombe zangu wanatoa maziwa mengi.” Kosa lililojitokeza katika tungo hii ni lipi kati ya haya? A Unyumbuaji wa maneno B Udondoshaji wa herufi C Unyumbuaji wa maneno D Upatanisho wa kisarufi E Uongezaji wa kiambishi (viii)”Serikali imeweka mikakati kabambe ilikupunguza umasikini.” Neno “ili” katika sentensi hii ni aina gani ya neno? A Kielezi C Kiwakilishi B Kiunganishi D Kihisishi E Kivumishi (ix) Mpangilio sahihi wa vipashio vinavyounda lugha ya Kiswahili ni upi? A Mofimu, kishazi, kirai, neno na sentensi. B Movimu, neno, kirai, sentensi na kishazi. C Neno, kirai, Kishazi, sentensi na mofimu. D Neno, mofimu, kirai, kishazi na sentensi. E Mofimu, neno, kirai, kishazi na sentensi. (x) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi? A Muundo wa kazi husika. B Wahusika wa kazi husika. C Jina la kazi husika. D Jina la mtunzi wa kazi husika. E Mtindo wa kazi husika. 2. Oanisha maana za dhana za uandishi zilizo katika Orodha Akwa kuchagua herufi ya dhana husika katika Orodha B,kisha andika herufi husika katika kijitabu chakko cha kujibia. Orodha A Orodha B (i) Kujieleza kwa lugha fasaha, mpangilio mzuri wa mawazo na A Mantiki kutumia misamiati. B Mkato (ii) Kujenga fikra fulani katika kifungu cha maneno. C Uandishi (iii) Mpangilio mzuri wa mawazo unaoeleweka kwa mwandishi na D Insha msomaji. E Wazo (iv) Kifungu cha maneno chenye kuelezea wazo maalumu, au sehemu F Aya ya wazo lililo katika mtiririko. (v) Alama ya uandishi inayotenga maneno yaliyo katika orodha G Kistari fulani. Ukurasa wa 3 kati ya 6
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org SEHEMU B (Alama 40) Jibu maswali yotekatika sehemu hii. Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org 3. Taja njia zilizotumika kuunda maneno yafuatayo: (a) Amirijeshi (b) Kiswahli (c) Kifaru (d) Chajio 4. Andika nahau yenye maana sawa na tungo zifuatazo: (a) Jumanne ni kijana mchoyo. (b) Yule ni mropokaji sana. (c) Malingumu ni mwizi. (d) Mwalimu wetu ameoa. 5. (a) Kwa kutumia njia ya mnyumbuliko, unda nomino mbili kwa kila kitenzi kifuatacho: (i) Piga (ii) Lima (iii) Pika (iv) Cheza (b) Tunga tungo moja kwa kila kipengele (i) - (iv) ukizingatia viambajengo vya kila moja: (i) Kishazi tegemezi + Kishazi huru (ii) Kishazi huru (iii) Kishazi tegemezi (iv) Kishazi huru + Kishazi huru 6. (a) Soma kwa makini sentensi (i) hadi (iv), kisha fafanua kwa pamoja vipengele vinne vinavyodhihirisha uhusiano baina ya Kiswahili na lugha za Kibantu. (i) Mtoto amelala (Kiswahili) (ii) Mwana agonili (Kingoni) (iii) Mwana yagonile (Kigogo) (iv) Omwana yanagila (Kihaya) (b) Kwa kutumia mifano na kutoa hoja mbili kwa kila moja, eleza kwa ufupi mafanikio ya lugha ya Kiswahli enzi za Waarabu katika: (i) Dini (ii) Biashara 7. Kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Takadinina Watoto wa Mama Ntilie,eleza kwa kifupi mambo manne ya kufanana kati ya wahusika Sekai na Mama Ntilie kuhusu wasifu wao wa ndani. 8. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata: Soni aliamka usingizini na kuendelea na safari yake. Awali alishtushwa na mitikisiko iliyotokea karibu na mbuyu. Hakujua yuko wapi lakini hakuchelewa kukumbuka nia ya safari yake. Aliukamata mkuki wake vizuri na ngao yake pia. Alipiga goti moja na kusimama hali akiuangalia mbuyu. Punde, Ukurasa wa 4 kati ya 6
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org aliwaona nyani wawili wakikimbilia nyasini. Wakasimama na kumtazama Soni. Naye alipoona hakuna hatari ya wanyama wakali, aliendelea na safari yake. Muda huo wa mchana ulikuwa salama kwani wanyama wakubwa walikuwa mapangoni mwao. Zaidi zilisikika sauti za panzi, nyenje na ndege tu waliojibizana kwa zamu. Soni alipumzika kidogo kwa mara nyingine ili kumnyonyesha mtoto. Hata hivyo, vivuli virefu vilimkumbusha kuwa usiku ulikaribia. Lakini hakusikia wala kuona dalili yoyote ile iliyoonesha kuwa binadamu waliishi katika eneo hili. Bado hakuelewa ni wapi alipokuwa. Ni kosa gani alilofanya? Je, mwanawe hakuwa binadamu? Ni kweli tofauti yake ni rangi tu? Hakuwa na vidole vya mikono na miguu vilivyomzidi baba yake. Macho yake na masikio pia yalikuwa sawa, aliyahesabu yote. Pale kila kitu kilipowekwa pamoja, mtoto alikuwa karibu sawa na wengine kuliko tofauti yake ya rangi tu. Sasa mbona wanataka kumuua? Soni alianza kukimbia kwa kasi kwani kama hangefika kijiji jirani, basi kutoroka kwake kungekuwa kazi bure. Punde si punde alishtushwa na mlio wa vipande vya miti vilivyovunjika. Soni alisimama akabana pumzi zake akisubiri sauti ile isikike tena. Huyo hakuwa mnyama mkali bali mtu aliyekusanya kuni. Upesi Soni aliharakisha upande ilikotoka sauti. Ghafla akamwona mzee mmoja akikusanya kuni. Alisogea kiasi ambacho kungetokea hatari angekimbia. Alimsalimia mzee yule. “Tafadhali kuwa mwema ili umsaidie mwanao aliyepotea,” alisubiri atakavyojibiwa. Kwa sauti ile yule mzee alizunguka na kuinua shoka lake kama ishara ya kutisha. Punde alipogundua kuwa aliyeongea alikuwa ni mwanamke, alipata ahueni na kulishusha shoka lake chini. Wakati ule Soni alisita na kuamua kusimama. Tumaini alizinduka usingizini. Huenda alihisi shaka iliyomkumba mama yake, akaanza kulia. Punde si punde, yule mzee alijiandaa kwa mashambulizi. Aliwaza kuna mtu nyuma ya yule mama. Iweje mwanamke mwenye mtoto mchanga aranderande msituni bila ya kuwa na mlinzi? Huenda anatumiwa na kijana imara aliyetaka kumuua. Wakati huo angefanyaje? Alikusanya kuni chache alizozipasua, akageuka ili aondoke. “Tafadhali usinitupe niliwe na wanyama wa usiku. Nisaidie! La, huwezi kunisaidia binti yako, basi msaidie mwanangu. Hajaonja maisha bado, na si vyema kufa sasa. Kilio mfululizo cha yule mtoto na maneno ya Soni vilimgusa yule mzee. Ingawa alisita, lakini hatimaye aligeuka nyuma. Kutokana na kauli yake, alihisi Soni alikuwa mgeni katika eneo hilo. Akaamua hata kama iweje, angemsaidia. Kwa hadhari kubwa aliwasogelea mama na mtoto wake. “Njoo mwanangu, tutakwenda kibandani kwangu.” Maswali (a) Pendekeza kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu. (b) Unafikiri kwa nini Soni alitoroka nyumbani kwake na kukimbilia msituni? (c) Mwandishi wa habari hii anaichukuliaje jamii ya akina Soni? (d) Kutokana na barai uliyosoma, eleza nafasi ya mwanamke katika jamii kwa kutoa hoja mbili. Ukurasa wa 5 kati ya 6
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org SEHEMU C (Alama 45) Jibuma swali matatu (3)kutoka katika sehemu hii. 9. Wewe ni mshiriki wa shindano la uandishi wa insha lililoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa. Kaulimbiu ya shindano ni “Watoto zingatieni daima maonyo ya wazazi wenu”. Kwa kutumia kauli mbiu hii, andika insha ya kisanaa isiyopungua maneno mia mbili (200) na isiyozidi maneno mia mbili hamsini (250), yenye kuishia na methali “Asiyesikia la mkuu huvunjika guu”. ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10-12 USHAIRI Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP) Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP) Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD) RIWAYA Takadini - Ben J. Hanson (MBS) Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P) Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P) TAMTHILIYA Orodha - Steve Reynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC) Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH) 10. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma, eleza jinsi taswira tatu kutoka katika kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii. 11. “Waandishi wa kazi za fasihi huibua migogoro mbalimbali na kupendekeza masuluhisho ili kuelimisha jamii husika”. Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika riwaya mbili ulizosoma. 12. Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma, fafanua madhara yanayotokana na kukosekana kwa elimu ya jinsia kwa vijana kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila kitabu. Ukurasa wa 6 kati ya 6