
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org
SEHEMU A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu maswali yotekatika sehemu hii.
1. Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Ingawa utaona kuwa haya nitakayoyasimulia hayakuhusu ndewe wala sikio, kwa vile mzigo wa
mwenzio ni kanda la usufi, lakini kumbuka, mwenzio akinyolewa na wewe tia maji maana
yaliyompata beku na ungo yatampata.
Ukiona yale yanayomsibu Mwanaheri hivi sasa ni dhahiri utakubaliana na mimi kuwa ujana ni kama
maua. Kwa matatizo anayoyapata Mwanaheri ni kuntu kuwa upigao ndio ufunzao. Ingawa kwake ni
sawa na maji yaliyomwagika hayazoleki, na ninaamini kuwa kwa wengine hili ni fundisho kwa
kuwa watu husema, kama hujui kufa tazama kaburi.
Uzee unaomkabili Mwanaheri sasa unahitaji msaada mkubwa wa mtoto wake haidhuru mjukuu
wake. Lakini maskini, hakupenda watu hao kuwa nao tangu awali ya maisha yake. Ingawa hivi sasa
anao watoto wa ndugu zake, lakini hawana msaada wowote kwake. Nidyo maana watu hawakukosea
kusema ndugu akizaa na wewe uzae maana changu si chetu. Hata wale mashoga zake waliokuwa
wakishirikiana naye katika kukata mitaa, wamemtupa Kigoma mwisho wa reli.
Kwa uzuri, alhamdulillah, aliumbika, maana alikuwa chuma hasa wala si masihara. Enzi zake
Mwanaheri, alikuwa Mwanaheri kweli. Alikuwa hapitwi na mwanamume. Mbali ya kuwa na kidevu
cha mfuto chenye kidimbwi kwa mbali, macho yake ya gololi yalimvuta mwanamume yeyote hata
muumini wa dini.
Miguu iliumbwa kadri ya mwili wake. Ukimwangalia kwa nyuma umbo lake ni sawa na umbo la
namba nane. Ingawa alikuwa na nywele za kipilipili, lakini alizitengeneza zikawa kama za singa.
Uzuri wote huo aliotunukiwa kama hedaya yake hapa duniani, umeathiriwa na mwenendo tu.
Mwenendo huu ulimpa jina baya la kuitwa jamvi la wageni.
Mwenendo huu ulikuwa sadfa ya ambacho kimekamilisha ule usemi wa wahenga kuwa uzuri wa
kuyu ndani imeoza au uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti. Alipokuwa kijana alikuwa hapendi
wachumba, wala watoto kwa kuchelea kutibua starehe zake. Kwa jinsi alivyokuwa anadanganyika
na ujana pamorja na rangi za dunia akifikiri atakuwa kijana mpaka kufa kwake. Alijididimiza katika
wimbi la starehe hadi akazama kiasi kwamba akalowana chapa. Naam! aliyetota hajui kutota. Mbali
na kutosikia la baba wala la mama, pia hakusikia la viongozi wa dini. Maisha yalikuwa dunia na
yeye na dunia. Ingawa alikuwa na wenzake katika shughuli hizo, lakini ni yale yale, yetu yetu,
yakikupata yako peke yako, lakini wenzako walikuwa wakifanya hayo na akili zao. Yeye
hakukumbuka kwamba nahodha mtweka chombo si mjinga wa bahari kwani mtu hufanya jambo
kwa akili zake, lakini Mwanaheri mwenzangu na miye hakuwa na hili wala lile. Wenzake hao sasa
wana watoto wao ambao wanawasaidia kwa moja au kwa jingine, wakati yeye anaumbuka. Kidagaa
kimemwozea. Mbali ya kuwa na ubao mara kwa mara, pa kuweka ubavu pia alipakiskia kwenye
bomba. Kwa mtu aliyeuona ujana wa Mwanaheri, hawezi kuamini kuwa ni huyu anayeahirika sasa
hivi. Naam! Asiyesikia la mkuu huvunjika guu, kama wanenvyo waneni, asiyefunzwa na mama
hufunzwa na ulimwengu.
Ukurasa wa 2 kati ya 5