
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org
SEHEMU A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Mipango ya elimu katika nchi mbalimbali duniani siku zote inahitilafiana, kimuundo na elimu
itolewayo. Mipango hiyo huhitilafiana kwa sababu nchi zenyewe zinazotoa elimu huhitalifiana, kwa
sababu elimu yoyote iwe ya darasani au si ya darasani, ina shababa yake. Shabaha yenyewe ni
kurithishana maarifa na mila za taifa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine na kuwaandaa vijana
wawe tayari kuchukua nafasi zao katika kulitumikia na kuliendeleza taifa. Hivi ndivyo ilivyo katika
nchi zote yaani nchi za kikabaila za Magharibi, nchi za kikomunist za Mashariki na hata
zilivyokuwa nchi za kiafrika kabla ya ukoloni.
Kwa hiyo, sio kweli kusema kwamba kabla ya ukoloni waafirka hawakuwa na elimu, eti kwa sababu
tu hawakuwa na shule, na kwamba makabila machache yalitoa mafunzo kwa muda mfupi tu
kambini. Watoto na vijana walijifunza kwa kuishi na kutenda. Nyumbani au shambani walijifunza
ufundi wa kazi zilizopaswa kufanywa, pamoja na tabia wanayopaswa kuwa nayo watu wa jamii ile.
Vile vile walifijunza aina za majani na mizizi ya miti ya porini, na kazi zake; walijifunza namna ya
kushughulikia mavuno na jinsi ya kuangalia mifungo. Haya yote waliyafanya kwa kushirikiana na
wale waliowazidi umri au wakubwa kuliko wao.
HIvyo jamii zilijifunza historia za makabila yao, na uhusiano baina ya kabila moja na makabila
mengine, uhusiano baina ya makabila yao na mizimu kwa kusikiliza tu hadithi zilizokuwa zikitolewa
na wazee. Kwa njia hii na kwa desturi za kushirikiana walizofunzwa vijana, tamaduni za nchi
ziliendelezwa. Kwa hiyo elimu waliyopata haikuwa y kukosekana kwa madarasa hakumaanishi
kwamba hakukuwako elimu, wala hakukupunguza umuhimu wa elimu katika Taifa. Kwa msingi
hiyo inawezekana kabisa kwamba elimu aliyokuwa akiipata kijana wa enzi zile ilikuwa elimu
inayomfaa kuishi katika jamii yake.
Huko Ulaya elimu ya darasani ilianza siku nyingi. Lengo la elimu hiyo ya Ulaya ilikuwa sawa na ile
iliyotolewa kwa mtindo wa asili wa Kiafrika, yaani, kwa kuishi na kutenda. Madhumuni makubwa
yalikuwa ni kuimarisha mila zilizokuwa zikitumika katika nchi, na kuwanadaa awatoto na vijana
kutimiza wajibu wao katika nchi hiyo. Na hivyo ndivyo ilivyo katika nchi za kikomunisti siku hizi.
mafunzo yanayotolewa ni tofauti na yale yanayotolewa katika nchi za Magharibi, lakini lengo likiwa
ni moja; kuwaandaa vijana kuishi katika taifa na kulitumikia taifa hilo, na kuendeleza busara, ujuzi
na mila za taifa katika kizazi kijacho. Mahali popote ambapo elimu inashindwa kutimiza malengo
hayo, basi maendeleo ya nchi hiyo yatalegalega, vinginevyo kutatokeo malalamiko watu
watakapogundua kwamba elimu yao imewaandalia kuishi maisha ambayo kwa kweli hayapo.
Maswali
(a) Eleza sababu mbili zinazosababisha nchi mbali mbali kuhitilafiana katika muundo wake
wa elimu.
(b) (i) Fafanua namna jamii za kiafrika zilivyokuwa zinatoa elimu kwa watu wake.
(ii) Ni nami waliohusika kutoa elimu katika jamii za kiafrika?
(c) Elimu iliyotolewa katika jamii za kiafrika na ile iliyotolewa huko Ulaya zilikuwa na malengo
gani?
(d) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma.
Ukurasa wa 2 kati ya 4