
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org
SEHEMU A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata. Nchi yetu ya Tanzania
imejulikana sana kutokana na mazingira yake yanayowavutia watalii. Hali yake ya hewa ni nzuri na
yenye kutamanika. Mvua yake si nyingi na haichukizi bali ni ya rasharasha
na tena ni ya hapa na pale. Majira yenyewe ya masika ni mafupi sana na hayana baridi kama huko
ulaya.
Kitu hasa kinachowavutia watalii kutembelea nchi yetu ni pwani zetu ambazo zina mchanga
mweupe na laini. Mchanga wenyewe hauna matope wala uchafu wowote. Kandokando ya pwani
hizo kuna vichaka vyenye miti yenye rangi chanikiwitina maua ya sampuli nyingi ya kutamanisha.
Maua hayo yapo ya rangi nyekundu na vilevile hunukia vizuri, ama huweza kuwa na rangi ya
manjano na kisha yakawa mviringo.
Kando kidogo unaweza kuona mawe makubwa yenye mapango makubwa mweusi ambamo
wanyama wakubwa na wakali kama chui huishi. Pengine hata wanyama wa kuchekesha na hata
watundu kama tumbili na kima huonekana humo.
Pembezoni, ambapo ni nje ya pwani zetu, kuna mashamba yenye mimea ya rangi ya kijani ikinawiri
hasa wakati wa masika. Kipindi hiki wakulima nao huwa wanajishughulisha na matayarisho pamoja
na maendeleo ya kazi zao za kila siku. Baadhi yao hupenda kufanya kazi huku wamevaa majoho
marefu meupe au pengine shuka za kaniki zilizochakaa. Aidha, wengine hawajishughulishi kamwe
na mambo ya mavazi kwani wao huvaa vikoi vikuukuu na vilivyokwajuka, bila kuja Zaidi ya pwani zetu, watalii
huvutiwa sana na mbuga zetu za wanyama wa porini. Wengi wa
wanyama katika mbuga zetu huwa na gozi zenye madoa ya rangi za kuvutia. Pengine hata maungo yao
huwa ya kutisha na yasiyokuwa ya kawaida. Mathalani ukimwona kifaru unadhani amekasirika na
kwamba anataka kukurarua vipande vipande. Simba naye anajulikana kwa makucha yake marefu ya
kutisha. Kiboko kwa upande wake, anajulikana kwa unene wake. Tumbo lake ni kubwa la kuchekesha
kwani kila umwonapo utadhani matumbo yataporomoka dakika yoyote. Basi mambo kama hayo na
mengine mengi, ndiyo yanayowavutia watalii kuja kwetu. Watalii hawa ambao wengine kati yao ni
warefu na pia wachangamfu lakini wapo walio wembamba na wepesi katika kuipanda milima yetu.
Hata hivyo, wapo pia wazee vikongwe wenye ari na nguvu katika kuipanda milima hiyo. Wote hawa
wanakuwa na hamu ya kutembelea vivutio vyetu. Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali, hurudi
kwao na furaha isiyo kipimo huku wakituachia fedha nyingi za kigeni.
Ukurasa wa 2 kati ya 5
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org