
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org
SEHEMU A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Ustaarabu ni jambo jema ambalo hupendwa na kila jamii yenye utashihapa duniani. Kila jamii
yenye ustaarabu mambo yake huendeshwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazoeleweka.
Maamuzi na mafanikio mbalimbali miongoni mwa wanajamii hutolewa bila hamakiwala
kukurupuka. Kanuni na taratibu hizo huiongoza jamii kufikia upeo wake kimaendeleo kuanzia
ngazi za chini kabisa ambayo ni familia mpaka ngazi ya juu kabisa ambayo ni taifa. Taratibu na
kanuni hizo huwekwa katika chombo kimoja maalumu kinachoitwa katiba.
Katiba ni jumla ya sheria, kanuni na taratibu fulani zilizokubaliwa kuwekwa na jamii au taifa
fulani kama dira ya maisha ya kila siku ya jamii au taifa hilo. Taifa bila katiba ni sawa na behewa
la garimoshi bila injini. Hivyo katiba ina umuhimu wa kipekee katika taifa lolote lile.
Katika nchi zenye utamaduni wa kidemokrasia, katiba huundwa kutokana na maoni ya wananchi
wake kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali. Aghalbu, maoni na mawazo yaliyotolewa na
wananchi huwa ni chimbuko la katiba hiyo. Wananchi hujiona ni sehemu ya utawala. Kwa upande
wa pili wa sarafu, nchi zenye utaratibu wa kiimla, katiba hutayarishwa na watawala kwa maslahi yao
binafsi. Katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala. Maoni na mawazo ya wananchi
hayazingatiwi katika kuunda katiba.
Umuhimu wa katiba huonekana na kujidhihirisha waziwazi katika maisha ya kila siku ya nchi
yoyote ile. Kwanza, katiba huelekeza wajibu wa ila mwanajamii kwa taifa lake na wajibu wa
viongozi walio madarakani kwa wananchi au raia. Pili, katiba huonesha na kuainisha haki ambazo
kila raia anastahili kupata na pia taratibu za kufuata katia kudai au dupewa haki hizo. Mbali na
hayo, katiba hutoa utaratibu wa jinsi ya kuwapata viongozi wetu katika ngazi mabalimbali za
kisiasa na kijamii. Pia uhuru wa mtu binafsi hulindwa na katiba. Hivyo, katika nchi ambayo ina
katiba inayokidhi matarajio ya wananchi wote mambo huwa mazuri na kamwe chombo hakiwezi
kwenda mrama.
Aidha, wananchi hawana budi kuelewa maana ya katiba ili waweze kutoa maoni na mapendekezo
ya kuunda katiba mpya au kuimarisha iliyopo. Ni muhali kwa mtu asiyejua maana ya katiba kutoa
maoni kuhusu katiba. Wananchi hupaswa kuelimishwa kupita semina, warsha na makongamano
mbalimbali ili kujua katiba zao na kutoa maoni kuhusu uundaji wa katibu mpya.
Hata hivyo, wananchi wengi hasa vijana hawajitumi katika kuzijua katiba za nchi zao au kutoa
maoni ya uundaji wa katiba mpya. Athari zake ni kutojua haki zao za msingi na kuburutwa kama
mkokoteni na watawala katika mambo mbalimbali. Vilevile hulalamikia mambo ambayo
hawakuchangia mawazo.
Hivyo basi, ni vizuri kwa wananchi kutambua, kuthamini na kuheshimu uwepo wa katiba kama
kiongozi kizuri katika kuonesha njia muafaka ya kujiletea maendeleo kisiasa, kijamii, kiuchumi na
kiutamaduni kwa nchi husika.
Ukurasa wa 2 kati ya 5