
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org
SEHEMU A (Alama 10)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
UFAHAMU
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Karibu masikio ya watu wa mahali pengi yalijaa habari za Karama na mashtaka yake. Umaarufu
wake wa ghafla ulizungumzwa karibu na mbali. Mtu yeyote wa desturi anapozuka katika umaarufu,
huyavuta masikio na macho ya watu wengi kwa sababu jambo kama hili hutokea nadra sana kwa
watu ambao bahati mbaya imeshughulika kuwaweka nyuma. Kwa hiyo, siku ya tatu ya baraza
ilihudhuriwa na mfalme, watu wenye vyeo mbalimbali, pamoja na nusu moja ya umati mkubwa wa
Kusadikika. Fikra zilizochanganyika ziliushika umati huu. Baadhi ya watu walimwajabia Karama
wakamhesabu kama mtu bora wa karne yao. Hawa walitumaini ataokoka lakini wengine waliwaza
kuwa Karama alikuwa kama mjinga aliyekuwa akicheza na hatari kubwa iliyofunua taya mbele
yake.
Waliokuwa wakimtazamia kuokoka walikuwa na wasiwasi wao; na wale waliokuwa wakimtazamia
kuanguka walikuwa na fadhaa yao. Walakini hapana mtu hata mmoja aliyepata kulisema wazo lake.
Bila ya kujua alivyoajabiwa Karama aliendelea kusema mbele ya baraza, “Watu wanaoteswa ndio
wanaoyajua mateso yao.” Kusadikika ilikuwa chini ya mateso makubwa sana. Maisha yao
yalizungukwa na maradhi na mauti, uadui usiokwisha, nchi iliyokaribia kugeuka jangwa na mwamba
na madhilamengine mazito yaliyowakabili watu. Wanakusadikika walitaka faraja katika mateso haya.
Kila jitihada ilijaribiwa ili kuirekebisha saa ya maendeleo ya nchi, lakini mara kwa mara majira yake
yalirudishwa nyuma. Kama hili lilifanywa kwa makosa ama kwa makusudi ni siri iliyo ng’ambo ya
fahamu zangu hata sasa. Lakini kama siri njema hufichika, ile iliyo mbaya haifichiki hata kidogo.
Uchaguzi wa wajumbe ulikuwako lakini hathibitisho ya matokeo ya ujumbe hayakupatikana.
Kusadikika iliishi kuona mjumbe baada ya mjumbe kuadhiriwa na kuadhibiwa vibaya. Kama
washauri hawakudhuriwa na hili lakini watu wengine walidhuriwa sana. Kazi njema za wajumbe
wawili zilipotea bure. Manung’uniko ya lawama hii yalikuwa katika hewa yote ya Kusadikika.
Hili lilipotokea serikali iliombwa ima faimakufanya ujumbe mwingine. Basi mjumbe wa tatu
alitakikana ajitolee mwenyewe kwa ujumbe wa Kusini. Wito wa mjumbe wa tatu uliitikiwa na
Kabuli; mtu mwenye busara, haya na mcheshi. Yeye alipatikana upesi kabisa kuliko ilivyokuwa kwa
mara ya pili na ya kwanza. Misiba ya Buruhani na Fadhili ilikuwa mikubwa ya kutosha kuikongoa
mioyo ya bidii katika bawaba zake. Kabuli aliyajua haya yote lakini alikuwa mtu wa moyo wa
namna nyingine kabisa. Alikuwa na bidii kubwa kama ile ya siafu athubutiye kukivuka kijito kwa
daraja iliyofanywa kwa maiti ya siafu wengine walioelea majini huko na huko. Maji yalijulikana
kuwa na asili ya rutuba, mvuke na umeme. Nguvu nyingine za namna mbalimbali zipo pia katika
maji. Kama siafu mdudu mdogo na kipofu wakati mwingine haogopi kuzikabili nguvu hizo pamoja
na hatari zake kwa sababu njema, basi ni dhahiri kuwa viongozi wa wanadamu wanapoteswa bure
bidii za wafuasi wao hutanuka ajabu.
Hapana tishio liwezalo kuukomesha mwendo huu. Kwa hakika utafululiza kuwako duniani mpaka
mateso yakome kabisa, na labda wakati huo dunia hii itakuwa njema kama itamaniwavyo kuwa.
Ukurasa wa 2 kati ya kurasa 5