
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org
SEHEMU A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Mtu hutembea njiani akajikwaa, ukucha ukang’oka au pengine hata kubwagwa chini vibaya na
kisiki, kisha mtu huyu hugeuka na akakiangalia kisiki hicho, ambacho pengine huwa hata
hakitazamiki.
Kama kisiki kimkwazavyo mtu atembeaye, pia mikasa mbalimbali, midogo kwa mikubwa,
huwakwaza na pengine hata kuwabwaga chini binadamu katika maisha yao. Jinsi baadhi ya mikasa
hii ilivyo adhimu, mtu anapokumbuka huweza kulia. Kwa upande mwingine mtu hujionea fahari
alivyopambana na mikasa hiyo kwa ujasiri hadi akaishinda au kuikwepa. Tukio kama hili hufanya
shajara la mambo bora ya kukumbukwa maishani.
Maisha ya shule ni mazuri, lakini mara nyingi huwa magumu na hasa lile wingu jeusi la mitihani
likaribiapo. Wanafunzi hupuuza sheria kama vile kwenda madarasani, michezoni na pengine hata
kula, wakajibanza mahali pa faragha wakajisomea. Nyakati zipendwazo ni usiku wa manane, kwa
kujua kuwa kila mtu amelala na kuwa hayupo mwalimu wa zamu awezayo kuzuru shule wakati huo.
Wanafunzi wenye bahati hunufaika sana kwa mpango huo wala hawagunduliwi. Wengine mara
hugunduliwa wakapewa adhabu ambayo huridhika kuifanya kwani nzi kufa kwenye kidonda si
hasara.
Siku hiyo ilikuwa Jumapili, nami nikajiunga katika ngoma ya kusoma na wenzangu wanne, wawili
wao walikuwa viranja wa madarasa. Ilipata saa nane za usiku nasi tukaingia katika chumba cha
kuoneshea picha, tukafunga mlango kwa funguo na komeo. Baada ya kuhakikisha kuwa hapana hata
mwonzi mdogo wa taa uliotambaa nje, tulitoa ala zetu, kila mtu akashughulika na hamsini zake.
Hapakupita saa moja, mara tunasikia mlango unabishwa hodi, “fungua mlango! tokeni sasa hivi.”
Sauti hiyo ilikuwa ya mmoja wa wanafunzi wa shule yetu. Mwanafunzi huyu aliandamana na mtu
ambaye tulimtambua kwa sauti kuwa alikuwa Tatu, dada mkuu wa shule. Mioyo ilianza kutudunda
kwa hofu, damu zetu zikawa karibu kuganda. Mara nilipata fahamu nikazima taa, lakini kwa bahati
mbaya chumba hicho hakikuwa na madirisha ambayo kwayo tungeliweza kutoka. Kumbe
mwanafunzi huyo naye alipata maarifa, alipanga viti kimoja juu ya kingine, akapanda juu na
kuchungulia ndani katika mwanya uliokuwa karibu na dari. Kumulika ndani akamtambua Dora.
Dora! Dora! fungueni mlango na tokeni sasa hivi!” akang’aka, lakini tukapiga kimya humo ndani.
Mwanafunzi huyo alipoona ameshindwa kututoa, alifanya hila ya kumwita mwalimu mkuu. Naam,
sauti ya simba huweza kumdondosha chini panya aliyejificha darini. “Dora fungua mlango sasa hivi!”
alinguruma, sote tulibaki tumeduwaa. Dora akafungua mlango, “ushikwapo shikamana” wahenga
walisema, mlango ulipofunguliwa mimi nilibana nyuma yake bila mtu kufahamu. Mwalimu mkuu
aliwasha taa akachungulia ndani. Kuona hakuna mtu alizima taa akaondoka zake kwenda kuwadadisi
wenzangu. Moyo ulishuka pwaa! nikatoka huku nagwaya mwili mzima, nikakimbia kwa mashaka
makubwa hadi benini kwangu. Kwa vyovyote vile nilijua nilikuwa ndani.
Ukurasa wa 2 kati ya 5