
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org
SEHEMU A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Misitu ya nchi ni mingi sana hata wakati mwingine tunadanganyika kuwa haitakwisha kamwe.
Tunaamini kwamba tunaweza kuendelea kuitumia miti yake na kuikata kwa ajili ya kupata mashamba
na malisho ya wanyama wetu bila kujishughulisha kupanda au kuhifadhi mingine kwa ajili ya siku za
mbele. Fikiria tulivyo na mawazo potofu. Fikira mbaya kama hizo wanazo watu wengi nchini mwetu.
Kwa hiyo imenilazimu kuwaonesheni kuwa misitu ni lazima ilindwe na haitalindwa kwa manufaa ya
kizazi chetu cha sasa tu, bali pia kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo.
Basi mjue kuwa kama misitu yote itakatwa patakuwa na upungufu mkubwa wa mbao na pia
upungufu wa maji ambao ni mbaya zaidi. Ubaya kama huu hautakiwi utokee katika Taifa letu
linalosonga mbele. Hatuwezi kuruhusu uharibifu wa misitu yetu uendelee kufanyika kwa sababu
unarudisha nyuma hali ya maisha yetu na unazuia ustawi wa nchi yetu. Hebu fikiria kwanza maisha
yetu yatakuwaje iwapo miti itakosekana - taabu ya kupika, gharama ya kujenga kwa chuma, mawe
au udongo ulaya badala ya miti. Gharama ya viti, vitanda na meza ikiwa vitatengenezwa kwa
chuma tu. Halafu fikiria kama maji yote yakikauka, ninyi nyote mwajua shida zitakazotokea, kwa
hiyo hatutaki kabisa shida kutokea.
Kwa nini tuwe na shida ya kukosa maji katika sehemu ambazo zina maji ya kutosha? Basi
inatupasa kuona kwamba kuna ulazima wa kuhifadhi misitu kwa ajili ya matumizi ya leo na kesho.
Bila shaka sasa utajiuliza mwenyewe. Je, siwezi kukata kabisa misitu ili niweze kulima? Jibu ni
kwamba unaweza kabisa, lakini ni katika sehemu zile ambazo hazikuhifadhiwa. Tena
ifahamike kwamba sehemu ambazo zimehifadhiwa ni chache sana ukilinganisha na mapori
makubwa yaliyobaki wazi kwa ajili ya kilimo.
Sasa nataka kusisitiza hasa juu ya misitu iliyohifadhiwa. Hizi ndizo sehemu za misitu ambazo ni za
lazima sana, na inatakiwa zihifadhiwe daima kwa matumizi ya faida ya Taifa. Misitu iliyohifadhiwa
ni misitu inayotazamiwa kudumu daima nchini. Inatunzwa ili itumiwe kwa utaratibu ulio bora kwa
kizazi hata kizazi. Kwa wakati ujao misitu hiyo itatoa mbao za kujenga nyumba, shule, hospitali na
majengo mengine, pia kutengeneza viti, meza, makabati, milango, madirisha na masanduku. Hata
sasa, mbao nyingi zitumikazo hutokana na miti iliyoota katika misitu iliyohifadhiwa. Lakini kwa
sababu ardhi yenye misitu ya aina hiyo inahitajiwa sana kwa kilimo, itatubidi kuanza kuotesha
misitu mipya kwa ajili ya mahitaji yetu. Basi ni lazima niwakumbushe wananchi kuwa miti iliyomo
katika misitu iliyohifadhiwa haitatosha kufanyia kazi zetu zote ili kuinua maisha ya watu na kuinua
uchumi wa nchi. Misitu iliyohifadhiwa lazima iongezwe kwa kupanda miti mingine, kwa mfano
hivi sasa Idara ya misitu inapanda miti kati ya eka elfu nne na tano kila mwaka na pia inaangalia
miti ya asili katika sehemu kubwa kabisa ya nchi hii.
Ukurasa wa 2 kati ya kurasa 4