Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION 021 KISWAHILI (Kwa Watahiniwa walioko Shuleni tu) Muda: Saa 3 Jumanne, 5 Oktoba 2010 mchana Maelekezo 1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E. 2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na D, swali moja (1)kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15ni la lazima. 3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali. 4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani. 5. Vikokotozi haviruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani. 6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia. Karatasi hii ina kurasa 5 zenye maandishi.
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org SEHEMU A (Alama 10) UFAHAMU Jibu maswali yote katika sehemu hii. 1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yatakayofuata: Sikukuu ya kusherehekea uvunaji wa viazi vipya ilikuwa inakaribia na Umuofia ilikuwa katika hali ya matayarisho. Hii ilikuwa ndiyo siku ambayo watu walitoa kafara kwa Ani, Mungu wa rutuba ya ardhi na mwamuzi wa mwenendo na uadilifu wa watu wote. Alikuwa Mungu aliyehusika sana na maisha ya watu na mababu wa Umuofia waliozikwa katika ardhi yake. Kwa sababu hii, sikukuu ilifanywa kila mwaka kabla mavuno hayajaanza. Hakuna mtu ambaye angeweza kula viazi vipya kabla havijatolewa sadaka kwa Ani au Mahoka wa mababu wa Umuofia. Watu wote waliifurahia siku hii na kuingoja kwa uchumkubwa kwa sababu yalikaribia majira ya vyakula maridhawa mwaka mpya. Watu wote waliokuwa na viazi vya mwaka uliopita ilibidi wavitupilie mbali kabla ya sikukuu hii haijaanza. Mwaka mpya ulitakiwa kuanzwa na vyakula vipya vilivyo vinono. Haikuwa heshima wala jambo la faraja kuendelea na vile vilivyokauka kutoka mwaka jana. Hata vyombo vya kupikia na vya kulia vilioshwa barabara. Kinu kile ambamo viazi vipya vilitwangwa kililazimu kusuguliwa sana. Sikukuu ya viazi lilikuwa tukio la nderemo Umuofia nzima. Yeyote aliyekuwa na mkono wenye nguvu kama wazee wasemavyo alitegemea kualika wageni wengi kutoka karibu na mbali. Okonkwo aliwaalika ndugu wa wake zake na kwa sababu alikuwa na wake watatu, wageni hao walikuwa wengi wa kutosha. Lakini ingawa hivyo, Okonkwo hakuwa mtu wa kufurahia sikukuu za aina yoyote. Ni kweli kwamba yeye aliweza kula sana, hata alipokunywa tembo alimaliza vibuyu vikubwa lakini kule kukaa bure bila kazi ndiko kulikomfanya asiwe na furaha. Furaha yake ilikuwa katika kazi ya shamba. Sasa sikukuu ilikuwa imekaribia na wake zake Okonkwo walisugua kuta za vibanda vyao kwa udongo wa aina mbalimbali. Wao wenyewe walijipamba kwa kuchorachora matumbo yao na migongo. Wageni wengi walikuwa wamealikwa hata Ikemefuna alikuwa katika shamrashamra hiyo. Kwao pia kulikuwa na sikukuu kama hii lakini hapa ilionekana kubwa na ya kufana zaidi. Na kwao sasa kilikuwa kitu kilichoanza kupotea katika dunia ya kumbukumbu yake. 2
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org Maswali (a) Eleza sababu mbili (2) zilizowafanya wananchi wa Umuofia waisubiri kwa uchu mkubwa siku iliyoelezewa kwenye kifungu cha habari. (b) Kwa mujibu wa kifungu cha habari, eleza sifa moja (1) iliyomtofautisha Okonkwo na watu wengine wa Umuofia. (c) Eleza maana ya maneno au kifungu cha maneno kilichokolezwa wino. (d) Unafikiri ni sababu ipi kubwa iliyosababisha kutupwa kwa viazi vyote vya zamani na vyombo vyote kuoshwa? (e) Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matano (5) kinachofaa kwa habari uliyosoma. 2. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha andika ufupisho wa maneno sitini (60) kuhusu habari hiyo. Kwa miaka mingi baadhi ya mila na desturi zetu zimetufunga hadi kutufikisha mahali ambapo imekuwa ni vigumu kwetu kubaini ukweli kuhusu mambo muhimu yanayotuzunguka, yakiwa ni yale yanayohusu sisi na miili yetu na yale yaliyonje ya miili hii. Kwa mfamo hadi leo kuna watoto wa umri mkubwa kufikia miaka saba ambao hawajui majina ya baba au mama zao. Lakini pia kuna vijana wa umri wa kuvunja ungo au balehe ambao hawajui ni kwa vipi mtoto anapatikana hasa maeneo ya vijijini. Kuna watu wazima ambao hadi leo mjadala kuhusu kifo ukiingizwa kenye mazungumzo huwa hawako tayari kusikiliza wakiamini kuwa huo ni mwiko na uchoro mkubwa. Hali hii kwa sehemu kubwa inatokana na desturi na mila zetu ambazo zimepogoka na zinahitaji kutazamwa upya kama zina faida kwa jamii. Baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakichukuliwa kama mwiko mkubwa kuyajadili hadharani au hata kati ya watu zaidi ya mmoja ni yale yanayohusu mbegu za kiume, yai la mwanamke na upatikanaji wa mimba. Siyo jambo la siri kwamba mada zenye kuhusu mambo haya ni nadra sana kujadiliwa katika jamii zetu na wengi ni maamuma kabisa kuhusiana na masuala haya. Inawezekana ikawashangaza wengi pale mtu atakaposema kuwa mwanamume anaweza kumpa mimba mwanamke bila mwanamume huyo kukutana kimwili na mwanamke anayehusika.
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA Jibu maswali yote katika sehemu hii. Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org 3. Eleza tofauti za msingi mbili (2) zilizopo kati ya kirai na kishazi. Toa mifano miwili kwa kila tofauti. 4. Ni kigezo kipi kinachotumika katika kuunda ngeli za kimapokeo? Dhihirisha utumiaji wa kigezo hicho kwa kutunga sentensi tano (5) za ngeli tofauti. 5. Kwa kutoa mifano, taja matumizi matano (5) tofauti ya kiunganishi “Kwa”. 6. Eleza tofauti kati ya viambishi awali na viambishi tamati. Toa maoni yako kuhusu dhana ya viambishi “kati” katika Kiswahili. 7. “Mofimu huru zina hadhi ya neno.” Fafanua usemi huu kwa kutumia sentensi tano (5) tofauti. SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii. 8. Eleza tofauti iliyopo kati ya hotuba na risala. Andika hotuba kuhusu “Maji ni Uhai.” 9. Wewe kama afisa ununuzi, andika barua kwa mfanyabiashara mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la bidhaa. SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI Jibu swali la kumi (10) 10. Kwa kutumia mifano, thibitisha ubantu wa Kiswahili kwa hoja madhubuti nne (4). 4
Mtihani huu na mitihani mingine inapatikana kwenye tovuti yetu: http://maktaba.tetea.org SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15ni la lazima. 11. Fafanua misemo ifuatayo: (i) Mungu si Athumani (ii) Kata mzizi wa fitina (iii) Mtu kidole (iv) Kondoo si mali (v) Kuiba kauli 12. “Kiongozi katika jamii ni nahodha ambaye hutakiwa aongoze chombo kisiende mrama.” Kwa kutumia hoja tatu (3) kutoka katika kila diwani jadili kauli hii ukitumia wasanii wawili uliowasoma. 13. Jadili jinsi fani ilivyotumika kukamilisha kazi za waandishi wawili (2) wa riwaya ulizosoma, ukizingatia mtindo na mandhari. 14. Waandishi wa tamthiliya wamemchora mwanamke katika sura tofauti. Thibitisha kauli hii kwa kutumia waandishi wawili (2) wa tamthiliya mbili (2) ulizosoma. 15. Tunga shairi la kimapokeo lenye beti nne (4) kuhusu unyanyasaji wa kijinsia. ORODHA YA VITABU Ushairi Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP) Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP) Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D. LTD) Riwaya Takadini - Ben Hanson (MBS) Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P) Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P) Tamthiliya Orodha - Steve Raynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC) Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH) 5